Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijaji: Pelekeni bidhaa zenu EAC, SADC

Dkt Kijaji Awataka Wafanyabiashara Dodoma Kuchangamkia Fursa Kijaji: Pelekeni bidhaa zenu EAC, SADC

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imekishauri kiwanda cha kuzalisha nyaya za umeme pamoja na transfoma cha Elsewedy kuhakikisha kinapeleka bidhaa zake katika masoko ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) ili kukuza uchumi wake na Taifa.

Ushauri huo umetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji leo wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichoko eneo la Kisarawe 11, Kigamboni Dar es Salaam kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji na kusikiliza changamoto zao.

Amesema kiwanda hicho kilichofunguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kinazalisha bidhaa mahsusi kwa ajili ya kwenda nchi za Kenya, Rwanda, Afrika Kusini na hata Demokrasia ya Kongo, jambo ambalo ni la mafanikio makubwa kwa Watanzania.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Elsewedy kwa ukanda wa EAC, Ibrahim Qamar amesema kiwanda hicho kilichoajiri Watanzania zaidi ya 200 kilianzishwa ili kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha uzalishaji wa bidhaa hizo kwa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla na hata kupenya katika masoko mbalimbali duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live