Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijaji: Msifungie watu biashara zao

Dkt Kijaji Awataka Wafanyabiashara Dodoma Kuchangamkia Fursa Msifungie watu biashara zao

Sat, 28 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji amezitaka taasisi zote za serikali zinazohusika na ukaguzi na udhibiti kuacha kufungia biashara na viwanda, kwani kufanya hivyo ni kusimamisha uchumi wa nchi.

Kijaji alisema katika maonesho ya wafanyabiashara yaliyoandaliwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) jijini Dar es Salaam.

“Naomba nisisitize kwa mamlaka zote za serikali za udhibiti ziendelee kuruhusu biashara zifanye kazi hata kama kuna jambo hatukubaliani kati yetu wakati tunashughulikia jambo lile hatuna sababu ya kusitisha kusimamisha shughuli za biashara, ni kusimamisha uchumi wa nchi.

“Kwa hiyo ni muhimu sana tunapoelekea kuhitimisha utekelezaji wetu wa dira yetu ya maendeleo ya mwaka 2025 tusisitishe shughuli yoyote ya kiuchumi kwa jambo lolote lile, kwani mazungumzo ni msingi wa sisi kuwa na uchumi imara, ” alisema.

Alisema Rais Samia Suluhu Hassan, aliamua kuwabeba wafanyabiashara, pia kuwalea wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ambao wako ndani ya Tanzania, hivyo mamlaka na taasisi zisifanye mzaha na uamuzi huo.

“Una jambo lako muite muhusika kaa nae acha shughuli ya kiuchumi iendelee kutengeneza ajira kwa vijana wetu kuchangia kukua kwa uchumi wa taifa letu, naamini wamenisikia naomba niwaombe wafanyabiashara na wenye viwanda mliopo hapa na ambao hawapo.

“Nimekabidhiwa jukumu la kuratibu sekta hii, simu yangu iko wazi saa 24 taasisi yoyote ya udhibiti inayokuja kukufungia biashara hata kama ni saa nane usiku nipigie simu tushughulike ili uendelee kufanya kazi,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live