Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijaji: Kampuni nane za Kitanzania zinauza bidhaa AfCFTA

Dkt Kijaji Awataka Wafanyabiashara Dodoma Kuchangamkia Fursa Kijaji: Kampuni nane za Kitanzania zinauza bidhaa AfCFTA

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema, katika kipindi cha miezi sita makampuni 8 kutoka nchini Tanzania wameuza bidhaa zao kwenye nchi mbalimbali barani Afrika chini ya mkataba wa eneo huru la Biashara Barani humo (AfCFTA).

Akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi ya mkutano wa pili wa wanawake wafanyabiashara wa bara la Afrika Dkt. Kijaji amesema kati ya wafanyabiashara hao 8 wafanyabiashara watatu ni wanawake.

Dkt. Kijaji amesema, mafanikio yaliyofikiwa na wafanyabiashara hasa wanawake katika bara la Afrika yanatokana na uwepo wa fursa katika kufanya biashara eneo huru la Afrika chini ya mkataba wa AfCFTA.

Ameongeza kuwa katika siku tatu za mkutano huo, kutakuwa na nafasi kwa wanawake hao kueleza namna walivyofanikiwa kufikisha bidhaa zao katika nchi mbalimbali barani Afrika

Chanzo: www.tanzaniaweb.live