Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Kigoma mbioni kuwa kitovu cha uchumi Afrika Mashariki’

Biashara Kigomaaa ‘Kigoma mbioni kuwa kitovu cha uchumi Afrika Mashariki’

Tue, 29 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa Kigoma, Thobias Andengenye amesema kuwa mkoa wake umeanza kutekeleza mpango wa kuwa kitovu cha uchumi kwa nchi za Afrika Mashariki ambapo kwenye mwaka mmoja madarakani wa Rais Samia Suluhu Hassan mambo makubwa yamefanyika ili kufi kia lengo hilo.

Andengenye alisema hayo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa mwaka mmoja ambao Rais Samia amekuwa madarakani na kusema kuwa Mkoa wa Kigoma umepiga hatua kubwa ya utekelezaji wa miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo mkoani humo.

Alisema kuwa mkoa umefanikiwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ambapo kwa sasa mradi wa barabara za kiwango cha lami kilometa 350 ulioanza kutekelezwa awamu ya tano unaendelea kutekelezwa.

Sambamba na hilo alisema kuwa mkoa unatekeleza miradi ya umeme wa gridi ya taifa ukiwemo mradi wa kutoa umeme mkoani Tabora kupitia Nguruka Wilaya ya Uvinza, umeme wa gridi kupitia Nyakanazi Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wenye KiloVolt 400 na uzalishaji wa umeme kutoka Maporomoko ya Mto Malagarasi.

“Na kwa sasa tayari vijiji 224 kati ya 306 vimeshapatiwa umeme, mitaa 138 kati ya 176 na kwamba utekelezaji wa miradi hiyo yote unaufanya Mkoa Kigoma kuwa tayari kutekeleza mpango wa kuwa kitovu cha biashara kwa nchi za Afrika Mashariki,” alisema.

Kuhusu usafirishaji Ziwa Tanganyika, alisema serikali imetenga Sh bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo na meli ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani 2,800.

Alisema meli za Mv Sangara na Liemba zimekarabatiwa ili kuimarisha usafirishaji ndani ya ziwa hilo na kwamba miradi hiyo itaufungua Mkoa wa Kigoma kiuchumi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live