Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigoma kuanza kuzalisha Chikichi

382e41090b833fe167ef732b7635f800 Kigoma kuanza kuzalisha Chikichi

Fri, 18 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye amesema kuwa mkoa huo umejipanga kutekeleza agizo la serikali la kuongeza uzalishaji wa zao la Mchikichi ambapo tayari wakulima wameanza kupanda miche ya Tenera ambayo hutoa mafuta mengi.

Andengenye amesema hayo leo alipofanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya mkoani humo.

“Zao la Mchikichi ndio litawafanya wakulima wa zao hilo mkoani humu kuwana uchumi imara pamoja na kuongeza upatikanaji wa malighafi ya kutengeneza mafuta,” amesema Andengenye.

Naye Kusaya amesema kuwa Wizara ya Kilimo ipo katika mpango kabambe wa kutekeleza agizo la Waziri Mkuu linalotaka zao hilo kulimwa katika mikoa ambayo hali yake ya hewa inafaa ili kukabiliana na upungufu wa mafuta ya kula.

Chanzo: habarileo.co.tz