Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigamboni kujengwa soko la samaki, machinga

Samaki Bunju Sumu Kigamboni kujengwa soko la samaki, machinga

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kata ya kimbiji iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam inatarajiwa kujengwa barabara yenye gharama zaidi ya Shilingi milioni 88 ikiwemo ujenzi wa soko kubwa la samaki na soko la Wamachinga katika eneo la Somangila.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtenvu ametoa kauli hiyo, wakati wa kufunga kampeni katika kata ya Kimbiji, ambapo amesema barabara hiyo inatarajia kuanza kujengwa April mwaka huu.

Naye Mgombea udiwani kata ya Kimbiji, Maimuna Mwinyipingu amesema eneo hilo kumekuwa na maendeleo makubwa ambapo shule ya msingi ya Kimbiji Pagawa imekuwa na matokeo mazuri ya Ufaulu kwa Wanafunzi.

Kwa Upande wake Mstahiki meya wa manispaa ya Kigamboni, Ernest Mafumbo amesema tayari yameshaingia makubaliano kwa ajili ya kujenga soko la samaki eneo la Somangila pamoja na soko la Wamachinga eneo la Gezaulole

Chanzo: www.tanzaniaweb.live