Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigahe: Wawekezaji saidieni jamii, lipeni kodi

Pesa Fedhaddd Kigahe: Wawekezaji saidieni jamii, lipeni kodi

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawekezaji nchini wametakiwa kuhakikisha wanasaidia jamii inayowazunguka, kulipa kodi stahiki ya Serikali na kutoa ajira hasa kwenye maeneo waliyowekeza.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kagahe ameyasema hayo Mjini Babati mkoani Manyara leo Alhamisi Oktoba 19 akizindua maonyesho ya Tanzanite Manyara Trade Fair, yanayoendelea kwenye viwanja vya kituo cha mabasi cha zamani.

Maonyesho ya Tanzanite Trade Fair yanahusisha wawekezaji na wajasiriamali mbalimbali yamedhaminiwa na kampuni ya Mati Super Brands LTD inayozalisha vinywaji vikali iliyopo mjini Babati.

Hata hivyo, ameipongeza kampuni ya Mati Super Brands ambao ni wazalishaji wa vinywaji vikali kwa uwekezaji wa viwanda walioufanya pamoja na kushiriki kudhamini Maonyesho ya Tanzanite Manyara Trade Fair.

Naibu Waziri huyo amepongeza juhudi za Mati katika kuwekeza na kulipa kodi stahiki ya serikali hivyo wawekezaji wengine nchini nao wanapaswa kuiga hayo.

"Wawekezaji wengine waige mfano wa kampuni ya Mati Super Brands LTD ambayo inasaidia jamii inayowazunguka, inalipa kodi stahiki na kutoa ajira hasa kwenye maeneo waliyowekeza," amesema Naibu Waziri Kigahe.

Meneja masoko wa kampuni ya Mati Super Brands, Elvis Peter amesema kuwa kampuni hiyo itaendelea kuzalisha bidhaa zenye ubora wa kitaifa na kimataifa .

“Kampuni yetu imekuwa ni wadhamini wakuu wa maonyesho ya Tanzanite Manyara Trade Fair ambayo yanakutanisha wafanyabishara kutoka ndani na nje ya nchi,” amesema Peter.

Naye Elias Baha ambaye ni mjasiriamali amesema wawekezaji wengi zaidi waende kuwekeza kwenye mkoa huo ili jamii ipate ajira kama ilivyofanya kampuni ya Mati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live