Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kidatu wazungumzia uzalishaji umeme

Wed, 31 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kilombero.  Meneja wa kituo cha kufua umeme kidatu,  Anthony Mushi amemhakikishia Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani kuwa kuwa kiasi cha maji kilichopo katika bwawa la Kidatu kina uwezo wa kuzalisha umeme hadi  2019.

Mushi ametoa ahadi hiyo leo Jumanne Oktoba 30, 2018 baada ya Kalemani kutembelea kituo hicho huku meneja huyo akibainisha kuwa kina uwezo wa kuzalisha megawati 204.

Amesema mitambo minne ya kufua umeme katika kituo hicho imekuwa ikifanyiwa matengenezo kulingana na ratiba iliyowekwa.

Katika ziara hiyo Kalemani aliwasha umeme kupitia mradi wa majaribio wa umeme wa bei nafuu unaotekelezwa na Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) awamu ya tatu kwenye kijiji cha Katulukila wilaya ya Kilombero. 

Kalemani alimtaka mkandarasi aliyesambaza umeme huo kutoka kampuni ya Namis Corporate Limited kurudi eneo la mradi kufunga transfoma tatu zitakazotosheleza mahitaji katika kijiji hicho. 

Amesema kwa kiasi kikubwa tatizo la kukatika kwa umeme nchini limepungua, kwamba yamebaki maeneo machache ukiwemo mji wa Ifakara ambao bado una tatizo la kukatika kwa umeme. 

Amebainisha kuwa katika kukabiliana na tatizo hilo hasa kwa mji wa Ifakara,  Tanesco imepanga kujenga kituo cha kupoza umeme na ujenzi huo utaanza mwezi ujao.

 

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz