Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibano cha TBS kwa wafanyabiashara wadanganyifu

TBS Kibano cha TBS kwa wafanyabiashara wadanganyifu

Thu, 2 Dec 2021 Chanzo: ippmedia.com

Akizungumza wakati wa mahojiano jijini Dodoma, Ofisa Usalama wa Chakula wa TBS, Deus Deule, alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kuhariri tarehe za muda wa matumizi ya bidhaa ambazo muda wake umeisha Ili bidhaa hizo ziendelee kuwa sokoni.

Hivi karibuni TBS wakati wa zoezi la kuteketeza bidhaa za chakula na vipodozi sisizo na ubora zenye thamani ya Sh. milioni 26.4.

Bidhaa zilizoteketezwa zimetokana na kaguzi  zilizofanyika kwenye maeneo mbalimbali ya biashara ikiwamo maduka, maghala, hoteli, na stoo zilizoko katika Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma na Singida ambazo zinaunda kanda ya kati kwa TBS, Deule, alisema ni marufuku kwa wafanyabiashara kuhariri tarehe za mwisho  za muda wa matumizi ya bidhaa na ukaguzi unaendelea kufanyika ili kubaini wanaofanya vitendo hivyo.

Alisema wanaobainika hutozwa faini kwa kujibu wa kanuni za ada na tozo  za mwaka 2021, ambapo kiwango cha faini kinaanzia Sh. 500,000.

Katika zoezi hilo jumla ya kilo 4,056 zenye thamani ya Sh. 26,448,500 zimeteketezwa ikijumuisha bidhaa za chakula na vipodozi zilizoisha muda wa matumizi, zenye viambata simu na zile ambazo tarehe za mwisho wa tarehe za matumizi zimehaririwa.

Alisema uwepo wa bidhaa zilizoisha muda wa matumizi na zile zenye viambato sumu zinaathiri uchumi wa nchi pomoja na afya za watumiaji na bidhaa za chakula zilizoisha muda wake na zile ambazo tarehe za mwisho wa matumizi zimehaririwa  zinaathiri upatikanaji wa virutubisho vinavyotegemewa vinaweza kusababisha magonjwa ya muda mfupi na mrefu ikiwamo saratani.

Deule alisema kwa upande wa vipodozi hasa vile vyenye  sumu, athari zake ni za muda mfupi na mrefu ikiwamo kuathirika ngozi, macho, mfumo wa uzazi kwa kinamama, ukuaji kwa watoto na magonjwa ya saratani hasa ngozi.

Chanzo: ippmedia.com