Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibali 'Kijani Bondi' ya CRDB chatolewa

Kijani Bondi (600 X 483) Kibali 'Kijani Bondi' ya CRDB chatolewa

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya CRDB leo imekabidhiwa kibali cha kuuza Hatifungani ya Kijani "Kijani Bondi" ya miaka 5 yenye thamani ya dola za marekani 300 milioni sawa na Shilingi Bilioni 780 na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).

Kibali hicho cha kutoa hatifungani ya kijani kimekabidhiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela aliyeambatana na Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Ally Laay katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam.

Kibali hicho kinaifanya Benki ya CRDB kuwa ya kwanza nchini kutoa hatifungani ya kijani, na ya kwanza kwa ukubwa Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kijani Bond itarahisisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kufadhili miradi rafiki kwa mazingira na kuchochea ufikiaji wa Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDG).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live