Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya kuzitoza ushuru bidhaa za Tanzania, Uganda

KIPTOO TZW

Thu, 7 Jun 2018 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya mvutano wa miezi kadhaa ya bidhaa zake kutozwa ushuru mkubwa tofauti na mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Kenya imesema itaanza kufanya hivyo kwa bidhaa za Tanzania na Uganda kuanzia Julai Mosi.

Kuanzia Machi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na ile Uganda (URA) zimekuwa zikizitoza ushuru wa asilimia 25 bidhaa tamu kutoka Kenya kama vile pipi, chokuleti, juisi na ice cream. Katibu mkuu wa Wizara ya Biashara Kenya, Chris Kiptoo alisema baada ya mazungumzo yaliyofanyika kati ya pande husika ndani ya kipindi cha mgogoro huo, Serikali imetoa mwezi mmoja zaidi na endapo hakutakuwa na mabadiliko, kuanzia Julai, Kenya pia itaanza kuzitoza

ushuru huo bidhaa za Tanzania na Uganda.

Katibu mkuu huyo alisema timu za wataalamu watakaothibitisha kama bidhaa hizo zinatumia sukari ya viwandani iliyosamehewa kodi kutoka Tanzania na Uganda zitaingia nchini humo kuanzia Juni 11 ili kujiridhisha.

“Tunafanya uamuzi baada ya uthibitisho kufanyika. Ikibidi tutalipiza kisasi lakini lazima tujipe muda kabla ya kufanya hivyo. Tutafanya uamuzi huo Juni 30,” alisema Kiptoo.

kuhusisha viwanda vya bidhaa nyingine kama vile saruji, vilainishi vya mitambo, vipodozi na bidhaa za mbao ambazo mara nyingi zimekuwa zikipata vikwazo kuingia Tanzania. “Tanzania na Uganda wanayo orodha ya bidhaa wanazozishuku kutokidhi vigezo vya asili ya bidhaa (certificates of origin), hivyo kuzitoza ushuru kinyume na mkataba wa biashara huru wa EAC wa mwaka 2010,” alisema Kiptoo.

Tangazo hilo lilitoa msamaha huo kuanzia tarehe ya kutolewa kwake hadi Julai 31, 2017 likiruhusu kuingiza tani 9,000 za maziwa ya unga na sukari isiyo na kikomo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live