Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katavi wauza dhahabu ya Sh bilioni 53.3

9008739ad509eb6e91ed0546390aca61 Katavi wauza dhahabu ya Sh bilioni 53.3

Mon, 19 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI Mkoa wa Katavi kupitia soko la madini imekusanya na kuuza dhahabu yenye uzito wa kilo 505 na gramu 632 kwa zaidi ya Sh bilioni 53.3 kwa kipindi cha Julai 2019 hadi mwaka jana.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera amelielezea HabariLEO katika mahojiano maalumu yaliyofanyika jana kuwa mkoa huo ni wa tano nchini kwa uuzaji wa madini mengi.

Akifafanua alisema kutokana na mauzo ya dhahabu hiyo yenye uzito wa zaidi ya nusu tani, serikali imejipatia zaidi Sh bilioni 3.4 ikiwa ni mapato ya mrahaba ambayo ni asilimia sita na Sh milioni 533 ikiwa ni ada ya ukaguzi ambayo ni asilimia moja.

Aliongeza kuwa Halmashauri ya Nsimbo na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kwa pamoja zimenufaika kwa kupata Sh milioni 160.

"Niliporipoti katika mkoa huu kama Mkuu wa Mkoa mwaka 2019 nilikuta dhahabu iliyokusanywa na kuuzwa ilikuwa na uzito wa gramu 129 tu...

Lakini baada ya kuanzishwa rasmi soko la madini, Mkoa wa Katavi tumekusanya na kuuza ya dhahabu yenye uzito wa zaidi ya nusu tani yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 53,"alibainisha.

Chanzo: www.habarileo.co.tz