Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kariakoo yatoa masharti matumizi soko jipya

KARIAKOO Kariakoo yatoa masharti matumiz soko jipya

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Masoko Kariakoo (KMC) limesema maeneo ya biashara yatatangazwa kielektroniki na kwambwa wafanyabiashara wote wanaodaiwa na Shirika watapaswa kulipa deni ili kupata maeneo mapya yaliyo boreshwa.

Kaimu Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, Sigsibert Valentine amesema maamuzi hayo yanalenga kulifanikisha shirika kukusanya madeni ya muda mrefu yanayokadiliwa kufikia Sh milioni 497.77.

“Tunaenda kutumia mfumo wa kielektroniki wa TAUSI ili kuleta tija. Shirika litatumia mfumo huo kutangaza maeneo ya biashara na kukusanya mapato,” amesema Velentine.

Taarifa iliyotolewa na Afisa Uhusiano Mkuu wa Shirika hilo, Revocatus Kassimba amesisitiza shirika halitaruhusu mfanyabiashara kupata umiliki wa eneo la kufanyia biashara ikiwa anadeni la awali.

Rais Samia aliidhinisha Sh bilioni 28.03 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Soko la Kariakoo baada ya kuungua. Ujenzi wa soko hilo umefikia asilimia 93. Haikuwekwa wazi ni lini soko hilo litafunguliwa kwa ajili ya matumizi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live