Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kariakoo kufanya biashara saa 24

Kkoo Pic Taarifa Kariakoo kufanya biashara saa 24

Mon, 18 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema baada ya ujenzi wa soko la Kariakoo kukamilika biashara zitafanyika saa 24.

Makalla ameyasema hayo leo Jumatatu Julai 18, 2022 alipokutana na watendaji na viongozi wa mkoa huo kuzungumzia kampeni yake ya kuiependezesha Dar es Salaam.

Makalla amesema Dar es Salaam ni Jiji la biashara haoni ni sababu gani watu walale na kikubwa ni kutengeneza mazingira ili utekelezaji wa kufanya biashara saa 24 ufanyike.

"Tunakoelekea hata kabla ya soko halijaisha lakini tukajiridhisha mazingira yanaruhusu, Dar biashara itakuwa saa 24 na soko likiisha ndio kabisaa.

"Tunataka mtu anatoka Zambia anafika leo anafanya manununuzi yake muda wowote anaotaka na kuondoka," amesema Makalla.

Amesema ili kufanikisha hilo, kuna mpango wa kufunga taa kila eneo la Jiji hilo ambapo hakutajulikana ni mchana au usiku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live