Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanuni kuwezesha NFRA kununua, kuhifadhi sukari

Sukarisssssssssss Kanuni kuwezesha NFRA kununua, kuhifadhi sukari

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema marekebisho ya kanuni za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) yatafanyika kuiweka sukari kuwa sehemu ya usalama wa chakula.

Mbali na hilo, yatafanyika marekebisho ya Sheria ya Sukari Na.6 ya mwaka 2001 kwenye sheria ya fedha ya mwaka 2024 kwa ajili ya kuiwezesha NFRA kununua na kuhifadhi sukari kwenye Hifadhi ya Chakula ya Taifa ili kunusuru hali ya upatikanaji wake inapotokea kudorora kwa soko la bidhaa hiyo.

Hayo yamo katika hotuba ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka 2024/2025 aliyowasilisha bungeni jana Mei 2, 2024.

Amesema hatua hiyo inalenga kuondoa uhodhi kwa baadhi ya wenye viwanda, bila kuathiri dhamira ya Serikali ya kulinda viwanda vya ndani.

“Serikali itaendelea kuvilinda viwanda vya ndani na kuwalinda wakulima wa miwa lakini ulinzi huo hautakuwa kwa gharama ya kuwatesa Watanzania milioni 61.7,” amesema.

Kupitia Bunge, Bashe amewaeleza wamiliki wa viwanda nchini kuwa sukari ni chakula cha Watanzania masikini na ni suala la usalama wa nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live