Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni zilizofanya udanganyifu kufutwa

Biteko Aiagiza TPDC Kuandaa Mapango Wa Muda Mrefu Upatikanaji Wa Gesi.jpeg Kampuni zilizofanya udanganyifu kufutwa

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amezindua Kiwanda cha kuwekea mifumo ya kupasha na kutunza joto katika mabomba yatakayosafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga nchini Tanzania kupitia Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP

Zoezi hilo la uzinduzi limefanyika jana Machi 26, 2024 lililoambatana na Sambamba na Utiaji saini Mikataba Mitatu, ambayo ni ukodishaji wa eneo la kujenga Miundombinu ya kuhifadhi mafuta (Land Lease Agreement for Marine storage and Terminal Area) Kati ya TPDC na EACOP.

Awali akizungumza wakatiwa uzinduzi wa kiwanda hicho mkuu wa mkoa wa Tabora amesema uwepo wa mradi huo umechochea shughuri za kimaendeleo mkoani humo.

Mkurugenzi mtendaji kutoka wa Shirika la Maendeleo Petrol Tanzania (TPDC) Musa Makame amesema mpaka sasa asilimia 87% sawa na bilioni 701 kati ya bilioni 800 zimekwisha lipwa kwaajili ya utekelezaji wameadi huo huku mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha ameeleza faida za utekelezaji wa mradi huo ndani ya wilaya ya Nzega.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Steven Diabato, umetumia fursa hiyo kumpongeza Rais Samia pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Mseven kwa uwekezaji huo Mkubwa wa Bomba la Mafuta Ghafi Afrika Mashariki EACOP na kuunganisha Mstari kutoka Hoima Uganda Hadi Chongoleani Tanga.

Akizungumza wakati wa kuzinduzi wa Kiwanda hicho na kushuhudia Utiaji Saini, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Doto Biteko ameipongeza nchi ya Uganda kwa kushirikiana na Tanzania kuwekeza Mradi huo wa Bomba la Mafuta Ghafi ambalo litachochea uchumi wa nchi zote mbili na kuwaletea maendeleo wananchi na kueleza miradi mbalimbali yauhusiano baina ya nchi hizo mbili.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Biteko amewaonya Watanzania kutotumika na Makampuni ya Nje kufanya udanganyifu ili wapate kazi kwenye Miradi ya Kimkakati (Local Content) na kuwanyima fursa wazawa na kusema kuwa zipo baadhi ya kampuni ambazo zimekwisha futwa kutokana na udanganyifu huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live