Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni zaidi ya 60 kushiriki maonesho ya famasia Afrika Mashariki

GY3A9490 Kampuni zaidi ya 60 kushiriki maonesho ya famasia Afrika Mashariki

Fri, 26 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni zaidi ya 60 kutoka nchi mbalimbali duniani, tayari zimethibitisha kushiriki katika maonesho makubwa ya famasia yanayofahamika kama ‘Pharmatech East Africa’ yatakayofanyika Jijini Dar es Salaam, ukumbi wa Diamond Jubilee, Agosti 30-1 Septemba, mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na Rais wa Chama cha Wafamasia nchini [PST], Fadhili Hezekiah wakati wa warsha iliyohusu uelewa wa chama hicho na Waandishi wa Habari, Jijini Dar es Salaam, Ambapo amesema kuwa maandalizi yameshakamilika na hadi sasa tayari kampuni hizo zimethibitisha.

‘’Maonesho haya ni mahususi na muhimu kama Taifa kuweza kujitokeza kujionea kujifunza kwani ni ya kwanza na ya kipekee kwa Tanzania hasa sekta ya afya.

Tunategemea kuwa na kampuni zaidi ya 100, lakini hadi sasa kampuni 60 tayari zimethibitisha, hii ni hatua kubwa sana kwetu kama waandaji kwa ushirikiano na kampuni ya ETSIPL.’’ Alisema Rais wa PST, Fadhili Hezekiah.

Aidha, amewaomba wadau na watu mbalimbali ikiwemo Vyuo vya Famasia nchini, kujitokeza kwa wingi kujionea maonesho hayo kwani ni sehemu ambayo watajifunza na kupata mashirikiano.

‘’Maonesho haya yanakuja na vitu mbalimbali. Makampuni yataonesha bidhaa zao ikiwemo dawa, na vifaa tiba, tutaona dawa kuanzia hatu ya awali hadi inapokuja kuwa dawa…kutakuwa na vitu zaidi kutoka kwenye makampuni haya makubwa duniani, ikiwemo Bara la Ulaya, Asia na kwingine,

Tunaomba makundi mbalimbali waje na wajifunze na hata kuona namna ya kuwekeza sekta ya dawa’’ alisema Rais wa PST, Fadhili Hezekiah.

Kwa upade wake, Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ETSIPL ya maonesho ya kibiashara kutoka India, Bw. Digvijay Singh ambao wanafanya maonesho hayo kwa kushirikiana na PST, amesema kuwa, Tanzania imekuwa na bahati kubwa, kwani makampuni makubwa yanakuja kuonesha bidhaa zao ambapo itachagiza fursa za uwekezaji.

‘’Kampuni kubwa kutoka nchi kama India, Uganda, Misri, Kenya, Rwanda na nyingine nyingi Bara la Ulaya, zinakuja kuonesha bidhaa zao, dawa na vifaa tiba, ambapo pia itakuwa ni fursa za wao kuwekeza hapa nchini, hivyo wadau na watu mbali mbali waje waone ni bure kabisa’’ alisema Singh.

Aidha, maonesho hayo pia yanawezeshwa na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali kupitia Wizara ya Afya, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba [TMDA], Bohari kuu ya Dawa [MSD] na wengine wengi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live