Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni za kibiashara kuwania tuzo SDGs

Sdg Pic Kampuni za kibiashara kuwania tuzo SDGs

Tue, 28 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la UN Global Compact Network Tanzania limezindua mchakato wa kutafuta mshindi wa tuzo zitakazokuwa zinatolewa kila mwaka kwa kampuni za kibiashara zilizoonesha kwa vitendo mchango wake kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Mchakato huo umezinduliwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shaban kwa lengo la kuendeleza ushirikiano kati ya wadau wa sekta binafsi na Serikali katika utekelezaji malengo ya maendeleo endelevu.

Naibu Katibu mkuu huyo alisema UN Global Compact chapa ya Tanzania ambayo inajumuisha wadau wa sekta binafsi ni washirika muhimu wa Serikali ambao hufanya mapitio ya hiyari ya malengo hayo ya maendeleo endelevu. Also Read

Aliyeua mke na mtoto mchanga wa wiki mbili akutwa kichakani akiwa hoi Kitaifa Feb 28 2023 Aliyeua mke na mtoto mchanga wa wiki mbili akutwa kichakani akiwa hoi Kitaifa Feb 28 2023

“Mathalani mwaka 2019, Tanzania ilikwenda kutoa utekelezaji wake wa malengo na mwaka 2023, Tanzania inakwenda kutoa tena hivyo lazima ishirikiane na wadau mbalimbali na moja ya wadau muhimu ni sekta binafsi ambao wanatusaidia utekelezaji wake.

“Wadau hawa tumewaomba waangalie hii tuzo ya kibiashara inaweza vipi kusaidia utekelezaji malengo yetu ya kitaifa lakini haya malengo yamejumuisha malengo ya maendeleo endelevu, hii ni katika kubadilisha ulimwengu na katika kutekeleza hayo ndio kuna ajenda 2030,” alisema.

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la UN Global Compact Network Tanzania, Simon Shayo alisema tuzo hizo zinalenga kutathmini malengo 17 ya maendeleo endelevu ambayo Taifa hujipima kila mwaka.

Shayo ambaye pia ni Makamu Rais wa kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) anayeshughulikia maendeleo endelevu kwa upande wa Tanzania na Ghana alisema licha ya kwamba ulimwengu utapimwa ifikapo mwaka 2030 kuona nchi zimefikia wapi kwenye maendeleo hayo, kubwa linakalopimwa ni ubia.

Alisema lengo la 17 linaitaka Serikali na wadau sekta binafsi na wengine kuingia kwenye ubia wa pamoja katika kuhakikisha kwamba maendeleo yanayofanyika sasa, yanasaidia kuhakikisha kwamba hakuna makundi au nchi zinazobaki nyuma.

“Malengo ya Maendeleo yetu yatakapofika 2030 tunataka tuone uwazi, kupungua kwa umaskini na uboreshaji wa maisha ya watu duniani pote,” alisema.

Alisema maeneo hayo ambayo Taifa limepiga hatua ni elimu, maji na maeneo mengine wanaamini kufikia 2030 kama nchi inayoendelea itakuwa imepiga hatua kubwa.

Alisema UN Global Compact ingependa kampuni za kibiashara zitizame mwenendo wao ili lengo lisiwe faida pekee bali iwe faida endelevu kwa maaa kwamba faida ya kampuni na biashara zake zionekana kugusa watu.

“Pia zionekana kulinda dunia na vizazi vijavyo, zionekane kuleta ustawi kwa watu wote, zionekane ni biashara zinazojenga ubia na serikali na mwisho tunaamini biashara na sewrikali zitaleta maendeleo,” alisema Shayo.

Aidha, mbali na tuzo hizo alisisitiza kuendeleza kuwapo kwa mijadala kuhusu taarifa ya hiyari ambayo Tanzania ni moja ya nchi 42 ambazo zitatoa taarifa kwa hiyari kuonesha wamefikia wapi kwenye utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu itakauofanyika Julai mwaka huu nchini Marekani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live