Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni za bima zina imani na sekta ya fedha

13511 Kampuni+pic TanzaniaWeb

Fri, 24 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Licha ya kushuka kwa faida ya benki za biashara na taasisi za fedha, kampuni za bima zimesema zitaendelea kuwekeza kwenye sekta ya fedha.

Msimamo huo umetolewa na mkurugenzi wa kampuni ya Sanlam Life Insurance, Khamis Sulema alipozungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa kimataifa wa kampuni za bima za ukanda wa Afrika mashariki na kusini.

“Ni kweli imetuathiri kwa sababu pesa tunazopata huwa tunaziwekeza kupitia benki. Sasa kama ulikuwa unapata gawio la asilimia 14 sasa hivi tunapata chini ya hapo,” alisema.

Kwa miaka miwili iliyopita faida ya benki imepungua huku baadhi zikipata hasara hata kushindwa kujiendesha.

Pamoja na hali hiyo, Sulema alisema wataendelea kuwekeza kwenye benki ziada ya faida wanayopata. “Tunategemea hadi mwaka 2020 walau asilimia 15 ya Watanzania watakuwa wanatumia aina yoyote ile ya bima ikiwamo kupitia benki au kampuni za simu,” alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz