Kampuni ya Lake Agro Investment Limited inayowekeza wilayani Utete wilayani Rufiji mkoani Pwani imesema inatarajia kuzalisha tani 100,000 za sukari kwa mwaka mpango unaolenga kuondoa nakisi ya sukari hapa nchini na kiasi kingine kuuza nje ya nchi.
Pia kupitia mradi huo wa kilimo cha miwa Utete Taifa na Mkoa wa Pwani itapata kodi huku ajira za moja kwa moja zaidi ya 10,000.
Hayo yameelezwa na mwakilishi wa kampuni hiyo, Abubakar Nassor wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi huo kwa mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge jana Juni 19, 2022 alipotembelea eneo la mradi huo lenye ukubwa wa hekta 15 ambalo lote watalitumia kwa kilimo cha miwa.
Nassor ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo iliyopo Utete, kushiriki kwenye uchumi huo kwa kulima miwa ya kutosha na pia kwa wale wakulima wa nje kulima zao hilo la kutosha na wafanyabiashara kuleta huduma hiyo ili kupata kipato.
"Tunafanya kazi na tunapata ushirikiano mzuri kutoka kwa mkuu wa mkoa na tunapata sapoti kutoka kwa mkuu wa wilaya na hii inaonyesha kwa vitendo azma ya Serikali kuhusu Tanzania ya viwanda na kuhakikisha uzalishaji wa kujitosheleza wa sukari tunaoweza kuufikia ndani ya muda mfupi na ikiwezekana tuweze kusafirisha kwenda nje ya nchi, kwa hiyo tuna mshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan,"amesem Nassor