Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni yaahidi kuzingatia mkakati kutandawazi

8dcaf047c48606b18d512652fbd40273.jpeg Kampuni yaahidi kuzingatia mkakati kutandawazi

Mon, 15 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KAMPUNI ya Huawei imeahidi kuzingatia mkakati wake wa utandawazi licha ya shinikizo la nje.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Ren Zhengfei (pichani), ametoa mwito kwa utawala mpya wa Marekani kuja na sera za wazi zaidi kwa maslahi ya kampuni za Marekani na uchumi wa Marekani kwa jumla.

Hii ni kauli ya kwanza kutolewa na mwanzilishi huyo wa Huawei tangu mabadiliko ya utawala wa Marekani.

Ren alikuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari huko Taiyuan, Mji Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini mwa China wa Shanxi, baada ya kuzindua Maabara ya Ubunifu wa Madini.

“Biashara inanufaisha pande zote mbili. Kuruhusu kampuni za Marekani kusambaza bidhaa kwa wateja wa China ni nzuri kwa utendaji wao wa kifedha.”

“Ikiwa uwezo wa uzalishaji wa Huawei utapanuka, kampuni za Marekani zinaweza kuuza zaidi. Sote tutanufaika. Ninaamini utawala mpya utapima maslahi haya wanapofikiria sera zao,” alisema Ren.

Ren alisema Huawei inajenga thamani kwa ekolojia nzima na uchumi mpana.

Alitoa mfano kwamba kampuni hiyo imeunda mitandao ya 5G katika miji mingi huko Ulaya, Asia na Mashariki ya Kati na majaribio ya mtandao huo yamekuwa na ufanisi wa hali ya juu, huku ikifaidisha watumiaji wote kwenye mitandao hiyo.

"Ukweli kwamba watumiaji wa hali ya juu wanaweza kutumia iPhone 12 kikamilifu kwenye mitandao yetu ya 5G huko Ulaya ni ushahidi wa ubora wa mitandao yetu," alisema Ren.

"Kama binadamu tunavyoendelea kufanya maendeleo, hakuna kampuni inayoweza kukuza tasnia ya utandawazi peke yake. Tunahitaji juhudi za pamoja duniani kote," Ren aliongeza.

Serikali ya Marekani imekuwa ikifanya kampeni dhidi ya Huawei katika miaka miwili iliyopita ikidai vifaa vya Huawei vinaweza kutumiwa kupeleleza Wamarekani, bila kuwasilisha ushahidi wowote.

Huawei imekataa mara kwa mara madai hayo, na nchi zingine chache zimekubali shinikizo la Marekani, zinalenga zaidi kuhakikisha wafanyabiashara wote wanakidhi viwango vya kiufundi kwa usalama.

Ren alisema sasa anajiamini zaidi juu ya uhai wa Huawei kuliko ilivyokuwa awali.

“Tumepata njia mpya zaidi za kushinda changamoto zetu. Mapato na mauzo yetu mwaka 2020 yalikuwa makubwa kuliko miaka iliyopita," alisema.

Ren alisema mikakati mpya ni pamoja na utafiti na maendeleo na kukuza sekta ya viwanda ulimwenguni kote kuwezesha mabadiliko ya kidigitali na uwezo wake wa msingi wa Tehama ya Huawei.

Ren pia alisema maabara ya kisasa ya Ubunifu wa Madini itasababisha huduma bora kwa migodi kwa kutumia teknolojia ya 5G.

“Kwa kusaidia tasnia ya madini, tunaweza kukuza biashara yetu na kusaidia uzalishaji bora na salama katika migodi. Tunaweza pia kuwezesha wafanyakazi wa mgodi wa makaa ya mawe 'kuvaa suti na tai’ kazini," Ren alisema.

Matokeo ya biashara ya Huawei kwa miezi tisa ya kwanza ya mwaka 2020 yalionesha kuwa mapato yalikuwa jumla ya Yuan bilioni 671.3 (Sawa na Dola za Marekani bilioni 98.57), ongezeko la asilimia 9.9 kutoka ile ya kipindi hicho hicho kwa mwaka 2019.

Chanzo: habarileo.co.tz