Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni ya mafuta ya Saudi yaongeza faida kwa wanahisa licha ya kushuka kwa mauzo

Kampuni Ya Mafuta Ya Saudi Yaongeza Faida Kwa Wanahisa Licha Ya Kushuka Kwa Mauzo Kampuni ya mafuta ya Saudi yaongeza faida kwa wanahisa licha ya kushuka kwa mauzo

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Saudi Aramco imeripoti kushuka kwa kasi kwa faida, baada ya kampuni kubwa ya nishati kupunguza uzalishaji na bei ya mafuta kushuka kwa kasi mnamo 2023.

Faida yake ilishuka kwa asilimia 25 hadi $121bn (£91bn) baada ya mwaka uliovunja rekodi mnamo 2022.

Lakini takwimu hiyo bado ni faida ya pili kwa juu kuwahi kutokea kwa kampuni inayoungwa mkono na serikali.

Kampuni hiyo ilisema inaongeza malipo yake kwa wanahisa na kutafuta fursa za kuwekeza nchini China.

Faida ya hisa itaongezeka hadi $98bn, ongezeko la karibu theluthi moja ikilinganishwa na 2022, wakati iliweka rekodi ya $161bn katika faida, kutokana na athari ambayo vita vya Urusi na Ukraine vilikuwa nayo kwenye bei ya nishati. Bei ya mafuta ilifikia $130 kwa pipa mwaka wa 2022.

Serikali ya Saudi inamiliki karibu 95% ya kampuni hiyo, kwa hivyo faida kubwa ilisababisha ziada ya bajeti ya ufalme mnamo 2022.

Mnamo 2023 bei ya mafuta ilishuka hadi $85 kwa pipa. Zaidi ya hayo, Saudi Aramco imepunguza uzalishaji ili kusaidia kuimarisha bei ya mafuta, na kuwa changamoto zaidi kwa faida.

"Mnamo 2023 tulipata mapato yetu ya pili kwa ukubwa kuwahi kutokea. Uthabiti wetu na wepesi ulichangia mtiririko mzuri wa pesa na viwango vya juu vya faida, licha ya kushuka kwa uchumi," mtendaji mkuu wa Aramco Amin Nasser alisema katika taarifa.

Chanzo: Bbc