Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni ya Twiga yazipiga jeki h’shauri

Acacias Hurdles Tanzania Hurts Barrick Gold Q3 Output Migodi ya Twiga

Thu, 16 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KAMPUNI ya uchimbaji madini ya Twiga Minerals Corperation Limited, inayomiliki migodi miwili ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyanhulu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, imekabidhi hundi ya Sh. billioni 1.5 kwa Halmashauri mbili Wilayani Kahama.

Malipo hayo ni moja ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha Januari, 2020 hadi Juni , mgodi wa Buzwagi ukilipa Sh.bilioni 1.1 kwa Halmashauri ya mji wa Kahama, huku mgodi wa Bulyanhulu ukilipa Sh. milioni 376 kwa Halmashauri ya Msalala.

Akikabidhi hundi hiyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, Meneja wa migodi miwili ya Bulyanhulu na Buzwagi, Benedict Busunzu, alisema malipo hayo yanafanyika ikiwa ni kutekeleza hitaji la kisheria, lakini pia ikiwa ni sehemu ya mikataba ya makubaliano kati ya migodi hiyo na Halmashauri mbili husika.

Busunzu alisema malipo hayo yanalenga kutatua kero na kuboresha huduma mbalimbali katika sekta ya afya, elimu, maji katika jamii zinazozunguka migodi hiyo na ziweze kunufaika na uwapo wa migodi hiyo katika maeneo yao.

Alisema mgodi huo umekuwa ukitoa fursa endelevu za kiuchumi na maendeleo kwa jamii katika sekta za kilimo, ufugaji ikiwa ni kuinua uchumi wa wilaya na kuboresha maisha wananchi wanaoishi katika maeneo hayo.

“Tunafarijika sana kwa ushirikiano ambao tumekuwa tukiupokea kutoka kwa wananchi ambao walikuwa wakiibua miradi mbalimbali na serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo unasaidia kufanikisha juhudi zetu za kujenga jamii endelevu,” alisema Busunzu.

Akipokea hundi hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Macha alisema kazi zinazofanywa na migodi hiyo ni moja ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuzitaka Halmashauri husika kuzitumia fedha hizo kwa miradi iliyokusudiwa ambayo italeta tija na mabadiliko kwa wananchi, kwa kutatua kero na kuboresha huduma za jamii.

Macha alisema wananchi kwa sasa wanahitaji maendeleo hasa kwa kutumia wawekezaji waliopo na kuongeza kuwa fedha zilizotolewa na wawekezaji hao thamani yake iendane na miradi itakayokuwa imetekelezwa na halmashauri husika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live