Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni ya Twiga yakabidhi bil 1.6/- za huduma, ushuru

38d37e7468318cbfc93d388edd382be8 Kampuni ya Twiga yakabidhi bil 1.6/- za huduma, ushuru

Fri, 12 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KAMPUNI ya Madini ya Twiga imekabidhi hundi yenye thamani ya jumla ya Sh bilioni 1.631 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji wa kampuni kwa jamii (CSR) na ushuru wa huduma kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

Kaimu Meneja wa Mgodi wa Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni hiyo, Zuwena Senkondo alisema wamekabidhi Sh bilioni 1.265 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya CSR na Sh milioni 366 za ushuru wa huduma.

Zuwena alisema fedha hizo ni gawio ambalo kampuni ya Twiga imekuwa ikitoa kila baada ya miezi sita na fedha iliyokabidhiwa ni ya kipindi cha kuanzia Julai hadi Desemba mwaka jana.

"Kutokana na uzalishaji ambao sasa hivi mgodi umeanza kufanya, gawio limeongezeka baada tu ya kuanza uzalishaji ambao umeanza, hivi karibuni tutarajie kupata ushuru mkubwa zaidi hapo mbeleni kwa kuwa mgodi sasa hivi unaendesha shughuli zake kikamirifu," alisema.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale, Mariam Chaurembo alisema fedha fedha za ushuru wa huduma zitagawanywa katika maeneo matatu ambayo ni asilimia 40 kwa ajili ya maendeleo, asilimia 10 kwa ajili ya vijana, wanawake na walemavu, na asilimia zinazobaki kwa matumizi kawaida.

"Kwa kuona umuhimu wa maendeleo, tumepeleka milioni 200 kwenye sekta hiyo kati ya Sh. milioni 366, milioni 56 kwa vijana, wanawake na walemavu, na ile inayobaki ndiyo itatumika kwa matumizi ya kawaida ikiwemo kununua gari la elimu msingi.”alisema Churembo na kuongeza:

"Pesa hizi ambazo tumepokea leo ni kwa awamu ya kwanza kwa sababu tunapokea pesa mara mbili kwa mwaka, pesa hizi mgawanyo wake upo mara mbili kwa sheria yetu ya bajeti asilimia 40 kwa ajili ya maendeleo na asilimia 60 kwa shughuli za kawaida,".

Januari 24 mwaka jana Serikali ya Tanzania na kampuni ya Barrick Gold Corporation walisaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano yaliyounda kampuni ya Twiga Minerals Cooperation Limited.

Chanzo: www.habarileo.co.tz