Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni ya Total waamua kubadilisha jina

Total.jpeg Kampuni ya Total

Tue, 22 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya mafuta ya Total imetangaza mabadiliko kwenye jina lake na sasa inakuwa TotalEnergies ambapo uzinduzi wa jina na nembo mpya na kituo chake cha kwanza cha huduma ya umeme wa jua umefanyika leo Samora Avenue Dar es salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Nishati January Makamba, Balozi wa Ufaransa Tanzania Nabil Hajlaoui, Mwenyekiti Mtendaji VP Olagoke Aloui na wengine.

Pamoja na hotuba yake ya mabadiliko haya ya safari mpya ya mabadiliko ya nishati Mkurugenzi wa Mtandao wa Biashara wa TotalEnergies Marieme Sow pia aliwashukuru Wateja wote Nchini kwa imani yao na kuifanya TotalEnergies kuwa kampuni namba 1 ya mafuta Tanzania.

Waziri Makamba mbali na kuzungumzia umahiri wa TotalEnergies na miaka yake 50 hapa Tanzania pia alizungumzia kupanda kwa bei ya mafuta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live