Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni ya Tigo yaja na ‘Toa bei Ushinde’

96364 Pic+yes Kampuni ya Tigo yaja na ‘Toa bei Ushinde’

Wed, 19 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kampuni ya mawasiliano Tigo, leo imezindua promosheni ijulikanayo kama ‘Bid-2-Win’ au ‘Toa bei ushinde’ itakayowapa wateja nafasi ya kununua bidhaa mbalimbali kwa bei ya chini.

Katika promosheni hiyo wateja wateweza kujishindia zawadi zenye thamani ya hadi Sh5 milioni.

Zawadi hizo zinahusisha bidhaa za kisasa na za kibunifu zikiwemo simu janja aina ya Samsung A30, A70, A50, pamoja na Playstation aina ya Sony.Bei ya chini ya kuanzia ni Sh1000/-.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo, Ikunda Ngowi ambaye ni mtaalamu wa huduma za Kidigitali wa Tigo, alisema promosheni hiyo imelenga kutoa shukrani zao kwa wateja kwa kuendelea kutumia mtandao wa Tigo na pia kuwapa wateja jukwaa litakalowawezesha kununua bidhaa kwa bei pungufu.

“Tunafurahi kuzindua rasmi promosheni hii na tunaamini kuwa itawapa nafasi wateja wa Tigo kupata bidhaa za kidigitali kwa gharama nafuu, huduma hii ni ya haki na inampa kila mteja nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali kulingana na thamani yake,” alisema.

Promosheni ya Toa bei ushinde itawapatia wateja bidhaa kwa bei pungufu ili kuwapa nafasi ya kufurahia maisha kwenye ulimwengu wa kidigitali.

Pia Soma

Advertisement

“Kama kampuni ya kidigitali, tunatambua mahitaji ya wateja wetu na siku zote tupo mstari wa mbele kuleta suluhisho zenye kuboresha namna watu wanavyotumia huduma za mawasiliano. Huduma hii inamruhusu mteja kutoa bei ya bidhaa husika na kumpa nafasi ya kushinda.Tunaamini kupitia promosheni hii tutafungua njia kwa watanzania wengi kumiliki teknolojia za kidigitali,” alisema

Kimsingi, Toa bei na Ushinde ni huduma ambayo itampa nafasi mteja kushinda bidhaa aipendayo kila wiki.Huduma hiyo pia itapungumza makali ya bei za bidhaa na kuwapa nafasi wateja kumiliki bidhaa wazipendazo kwa gharama nafuu.

Ngowi aliwahimiza wateja kushiriki kwa wingi katika promosheni hiyo kwani kadiri unavyoshiriki ndivyo unajiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kushinda.

Chanzo: mwananchi.co.tz