Wadhibiti wa Usalama nchini Marekani wameishinikiza kampuni ya Tesla kuyarejesha karibu magari 363,000 yenye mfumo wa kujiendesha yenyewe "Full Self-Driving" kwa sababu hayazingatii utaratibu katika makutano ya barabara na pia vidhibiti mwendo.
Hatua hii ni sehemu ya uchunguzi mkubwa zaidi kuwahi kufanywa na Mdhibiti Mkuu wa Usalama Barabarani (National Highway Traffic Safety Administration - NHTSA) katika mifumo ya kiotomatiki ya mtengenezaji wa magari ya umeme,Tesla.
Hata hivyo, uamuzi huo umezua maswali kuhusu madai ya Mkurugenzi Mtendaji Elon Musk kwamba anaweza kuthibitisha kwa wadhibiti kwamba magari yenye "Full Self-Driving" ni salama zaidi kuliko wanadamu, na kwamba wanadamu kamwe hawapaswi kugusa vidhibiti.