Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni ya Sigara TCC yapata faida ya bilioni 23.9

Tumbaku Y Kampuni ya Sigara TCC yapata faida ya bilioni 23.9

Tue, 24 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya Sigara Tanzania TCC imepata faida ya asilimia 10% katika kipindi cha nusu mwaka wa 2021 kutokana na mazingira bora ya biashara na biashara ya sigara kutoathirika na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.

Katika taarifa yake ya kifedha katika kipindi cha miezi sita iliyotolewa, Hadi kufikia mwezi juni 30 2021 kampuni ya tumbaku ilisema ilipata bilioni 23.9 tofauti ya bilioni 21.6 iliyopata mwaka jana 2020.

Mwenyekiti wa Bodi ya TCC Bwn. Paul Mkanza alisema kuna uboreshaji wa kiwango cha mauzo yake, na mafanikio yalionekana kwenye gharama pamoja na mikakakati ya ufanisi iliyopitishwa na kampuni hiyo.

"Gharama za uendeshaji hazikubadirika, tumeonesha ufanisi na utendaji mzuri kwenye maeneo yote ya biashara na tumefanikiwa kuhifadhi pesa taslimu katika kipini chote hiki"

Kampuni ya Sigara TCC kwa sasa imepata matumaini kutokana na kazi nzuri iliyoonekana mwaka huu wa 2021 na ikiwa mazingira ya biashara yataendelea kuboreshwa, pamoja na hatua ambazo zimetangazwa na seikali hivi karibuni zitaendelea kuchukuliwa katika kuinua uchumi TCC itakuwa na uhakika wakufanya vizuri zaidi.

"Wakurugenzi wampata matumaini baada ya maotokea ya nusu mwaka na kuatarajia mengi zaidi ifikapo desemba 31 2021" alisema Bwan Makanza

Kwa mujibu wa TCC ilifanikiwa kuongeza mauzo ya ndani kwa asilimia 16.5 na nje kwa asilimia 3.7 kutokana na mazingia ya biashara kuimarishwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live