Kampuni ya Northrop Grumman Corp imezindua ndege yake mpya ya ufyatuzi wa mabomu aina ya B-21 “Raider” aina ya jet, ikiwa ni aina mpya iliyotengenezwa kwa chuma yenye uwezo wa kusafiri angani na kufyatua mabomu ya nyuklia kwa ajili ya kikosi cha anga cha Marekani, Air Force, imeripoti taarifa ya Reuters.
Ndege hiyo B-21 ilizinduliwa katika sherehe ya aina yake iliyofanyika kwenye kiwanda Northrop cha 42, kilichopo katika eneo la Palmdale, California, ili kutoa fursa kwa umma kuitazama kwa mara ya kwanza.
B-21, yenye muundo sawa na ule wa awali B-2 wa “bawa la ndege ” itaweza kufyatua silaha za kawaida na zile za nyuklia katika maeneo mbali mbali ya dunia ikiwa pia na uwezo wa kufyatua maeneo yaliyolengwa ya masafa marefu na mafupi angani.
Ndege hiyo ilikadiriwa kugarimu kiasi cha dola zipatazomilioni 550 kila moja katika mwaka 2010, au karibu dola milioni 750 kwa sasa kutokana na mabadiliko ya thamani ya dola.
Air Force inapanga kununua walau ndge za aina hii 100 na kuanza kuzitumia badala ya zile za awali za B-1.