Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni ya Marekani kununua Korosho zote kutoka Tanzania

Balozi123 Kampuni ya Marekani kununua Korosho zote kutoka Tanzania.

Thu, 26 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wasindikaji wa Korosho nchini Tanzania wametakiwa kuongeza uwezo wa kusindika korosho nyingi zaidi baada ya Kampuni ya WHI kutangaza kununua korosho zote zilizosindikwa na kuthibitishwa na Tanzania.

Kampuni ya Marekani ya World Holdings International (WHI) amesema imepata kampuni ambayo itanunua bidhaa kutoka Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya WHI aliitaja kampuni hiyo kuwa ni JF Braun and Sons ambayo itafanya manunuzi ya bidhaa za Tanzania.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Bwan. Ward amesema kmpuni ya JF Braun & Sons ni kampuni inayoongoza kwa kununua na kusambaza matunda makavu na karanga katika soko la Marekani.

Bwan. Ward amesema kampuni hiyo inashirikiana na kampuni Tanzu ya Gellert Global Group ambayo huuza na kununua bidhaa za chakula kwa zaidi ya dola bilioni 1 kila mwaka Marekani.

"Kontena la kwanza limepangwa kuondoka Dar Es Salaam kwenda marekani kabla ya mwisho wa mwaka huu" alisema Bwn. Ward

Bwa. Ward amesema kama kila kitu kitaenda sawa, Wawekezaji wataweza kununua kilo 1 ya korosho za kusindikwa kwa Dola 6.7 sawa na shilingi 14,950 ambayo ni kubwa ukilinganisha na bei iliyopo soko la dunia ambapo kilo moja inauzwa kwa dola 5.60 sawa na shilingi 12, 880

Katika msimu wa mwisho uliopita korosho ghafi iliuzwa kwa shilingi 1900 kwa kilo na 27,00.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live