Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni ya Jumia yafunga biashara Tanzania

86368 Jumuyapic Kampuni ya Jumia yafunga biashara Tanzania

Fri, 29 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kampuni ya teknolojia ya Jumia Tanzania iliyokuwa ikitoa jukwaa la kununua na kuuza bidhaa mbalimbali imefunga biashara zake nchini kwa maelezo kuwa hakuna manufaa inayoyapata.

Novemba 18, 2019 kampuni hiyo ambayo makao makuu yake yapo nchini Nigeria ilifunga biashara zake katika nchini Cameroon kwa sababu kama hizo.

"Kwa kuzingatia tathmini yetu ya kuelekea mafanikio, tumefanya maamuzi magumu ya kusitisha shughuli zetu  Tanzania kuanzia Novemba 27, 2019.”

"Tanzania kuna fursa kubwa lakini tumeona ni vyema kutumia rasilimali zetu katika masoko mengine, uamuzi huo sio rahisi lakini unatusaidia kuweka mkazo na rasilimali zetu mahali ambapo tunaweza  kuleta matunda na kusaidia ustawi wa Jumia,” inaeleza sehemu ya taarifa ya Jumuiya hiyo.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa waliojiunga na jukwaa hilo wataendelea kulitumia lakini hakutakuwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Kampuni hiyo ipo nchini Nigeria, Misri, Morocco, Kenya, Ivory Coast, Afrika Kusini,  Tunisia, Algeria, Ghana, Senegal, Uganda, na Rwanda.

Chanzo: mwananchi.co.tz