Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni ya Chalinze Cement yalalamika kufutia usajili

Sdga Kampuni ya Chalinze Cement yalalamika kufutia usajili

Tue, 9 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku chache baada ya Serikali kutangaza kuwa Chalinze Cement ilifutwa kwa mujibu wa sheria kutokana na kutoa taarifa za uongo wakati wa usajili wake, kampuni hiyo imedai kuwa haikupewa nafasi ya kusikilizwa.

Hayo yamesemwa na wakili wa Chalinze Cement, Melchisedeck Lutema wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kutangazwa kufutwa kwa kampuni hiyo na msimamo wao juu ya kuendelea kupinga muunganiko wa kampuni ya Tanga Cement na Twiga kwa kile alichoeleza kuwa unavunja sheria.

Kauli yao pia imekuja ikiwa ni siku chache tangu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Dk Ashantu Kijaji kuliambia Bunge kuwa kampuni ya Chalinze ambayo imekuwa kinara kupinga muunganiko huu ilifutwa kisheria baada ya kubainika kutoa maelezo ya uongo wakati wa usajili na kushindwa kujieleza ndani ya siku 30 walizopewa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live