Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni ya Apple kuja na 'Lockdown Mode'

LI IPhone Lockdown Mode.jpeg Kampuni ya Apple kuja na 'Lockdown Mode'

Tue, 12 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya Apple imetangaza mfumo wake mpya uitwao ‘lockdown mode’ ambayo itapatikana katika iOS 16 kwenye simu za iPhone pamoja na iPads, uliopangwa kuzinduliwa baadae mwaka huu.

‘Lockdown mode’ ni mfumo unaolenga wale watu ambao vifaa vyao viko hatarini zaidi kudukuliwa na hii ‘lockdown mode’ itafanya iPhone kuwa moja ya simu salama zaidi zinazopatikana sokoni.

Inasemekana kuwa simu yako ya iPhone ikiwa kwenye hali ya lockdown, hata Serikali ya Marekani haitoweza kuifikia taarifa katika simu bila ridhaa yako.

Ili kuhakikisha kuwa inabaki hivyo, Apple inatoa zawadi ya hadi $2,000,000 (Tsh. 4,662,000,000) kwa wadukuzi ambao wataweza kupata njia za kuepuka huo mfumo wa ‘lockdown’ na kuidukua simu yako, hii imefanywa kama njia ya kuongeza umadhubuti wa mfumo wao mpya.

"Apple hutengeneza vifaa vya simu za mkononi vilivyo salama zaidi kwenye soko," Ivan Krstić, Mkuu wa Uhandisi wa Usalama na Usanifu wa Apple, amesema katika taarifa na kusema Lockdown mode’ ni uwezo wa msingi ambao unaonyesha dhamira yetu ya kulinda watumiaji dhidi ya shambulio la udukuzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live