Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni tatu zavuka lengo utoaji gawio

12002 Kampuni+pic TanzaniaWeb

Mon, 23 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kampuni tatu za Serikali zimevuka lengo la gawio kwa Serikali kwa mwaka 2017/18, kati ya 47 zilizowasilisha leo Julai 23, 2018 kwa Rais John Magufuli.

Akizungumza wakati wa mkutano maalumu kwa wakala, kampuni, taasisi na mashirika ya umma, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema gawio hilo litaiwezesha Serikali kuboresha huduma mbalimbali za jamii.

Waziri Mpango amezitaja kampuni hizo kuwa ni Mamlaka ya Ngorongoro iliyoweka lengo la kutoa Sh13.24bilioni na wametoa Sh22.35 bilioni, Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) ShSh30.69 bilioni na imekusanya Sh59.86 bilioni na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) Sh30.77 bilioni na imeikabidhi Serikali Sh34.74 bilioni.

Hata hivyo, Dk Mpango ametoa onyo kwa mashirika  ambayo hayajawasilisha gawio serikalini na kuyataka yajitathmini.

“Wakuu wa taasisi na mashirika mliopo humu ambao hamjaleta gawio mjitathmini na kuwa wale wawekezaji wote ambao hawajatoa pia wajitathmini,” amesema Waziri Mpango na kuongeza:

“Zipo changamoto zinazofanya wamiliki na wakuu wa taasisi kushindwa kukamilisha hili, sababu kubwa ni usimamizi dhaifu usioridhisha na gharama kubwa za uzalishaji, tunachokifanya sasa ni kuimarisha ofisi ya msajili wa hazina kibajeti ili kufikia lengo.”

Chanzo: mwananchi.co.tz