Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni tano zaonyesha nia kuwekeza usafiri wa reli Dar

RELII Kampuni tano zaonyesha nia kuwekeza usafiri wa reli Dar

Sat, 16 Sep 2023 Chanzo: Mwananchi

Dar es Salaam. Zaidi ya kampuni tano zimeonyesha nia ya kuwekeza katika miundombinu ya reli kwa ajili ya usafiri wa treni ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Hayo yalisemwa jana na Kamishna wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), David Kafulila, alipokuwa akisikiliza mawasilisho ya wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi, wenye nia ya kuwekeza nchini, utaratibu ambao huufanya kila siku ya Alhamisi na Ijumaa.

Akizungumza na waandishi mara baada ya kumaliza kusikiliza mawasilisho hayo, Kafulila amesema makampuni mengi yameonyesha nia ya kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo ya usafirishaji na moja ya eneo waliovutiwa nalo ni la miundombinu ya reli ndani ya Dar es Salaam.

“Sasa hivi kampuni hizi tumewaambia waende wakafanye uchambuzi wa awali wa mradi (pre fercibility study), ili wakiyaleta yapitiwe kwa hatua za awali kabla yakwenda kwenye maandiko yaliyokamilika (comprehensive fercibility study), na kutokea huko kuamua kama hilo andiko lipo sawa au la,” amesema Kafulila.

Akifafanua zaidi, Kafulila amesema makampuni hayo yamevutiwa kuwekeza katika eneo hilo, kutokana na kuona Dar es Salaam inakabiliwa na tatizo kubwa la foleni.

“Unajua kila siku Dar es Salam inapoteza Sh4 bilioni kwa hiyo kwa mwaka unazungumza kama Sh1.4 trilioni kwa sababu ya foleni tu na hii inatokana na muda unaotumiwa watu wakiwa barabarani kuwahi sehemu zao za kazi na mafuta yanayotumika katika vyombo vya usafiri,“ ameeleza Kafulila.

Uwekezaji mwingine katika sekta ya usafiri unaoangaliwa, Kafulila amesema ni miundombini ya mabasi yaendayo haraka (BRT), pamoja na barabara za kuwatoa watu pembezoni mwa jiji kazi inayofanywana Wakala wa Barabara nchini (TANROAD).

Akielezea kusudi la kukutana na wawekazaji hao, Kafulila amesema inatokana na Serikali kuwa na mpango wa miaka mitano wa miradi ya maendeleo, unaogharimu Sh114 trilioni kwa tathimini ya mwaka 2021; na kubainisha kuwa, katika mpango huo, Sh40.3 trilioni iliapangwa itokane na sekta binafsi.

Mmoja wa wakezaji, Janita Ferentinos, amesema hivi sasa wanashukuru kumekuwa na mabadiliko katika uwekezaji ikiwemo kufikiwa na miundombinu ya barabara, maji na umeme.

"Zamani ilikuwa unaanzisha kama ni kiwanda unamaliza lakini miundombinu ya kupelekwa umeme inakuwa ni shida kwa kweli tunashukuru kwa sasa kumekuwa na mabadiliko katika eneo hilo," amesema Jane.

Chanzo: Mwananchi