Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni sita za bima kuilipa Gulf fidia ya Tsh bilioni 1

Gulf Pic Kampuni sita za bima kuilipa Gulf fidia ya bilioni 1

Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni sita za bima zimeshindwa kesi ya kisheria iliyotolewa maamuzi na Mahakama Kuu ya Tanzania ya kuzitaka kulipa jumla ya shilingi bilioni 1 kampuni ya Gulg Petroleum kama fidia iliyosababishwa na kumwagika kwa mafuta yaliyokuwa yakisafirishwa katika tanki maalum la kufidhia bidha hiyo maeneo ya Kurasini jijini Dar es Salaam.

Baada ya kutoridhishwa na maamuzi hayo, kampuni hizo zilikata rufaa kupinga kulipa kiasi hicho cha fedha, maombi ambayo yamegonga mwamba katika Mahakama ya Rufaa Dar es Salaam.

Mahakama Kuu ilisisitiza kuwa hitilafu hiyo ilisababisha upotevu mkubwa mafuta kwa kamuni ya Gulf na kuwa ni haki yao kulipwa na kampuni hizo za bima na kuwa katika mkataba waliongia unaoesha kuwa Kampuni hizo zitawajibika katika suala hilo.

Gulf ilikata bima ya mwaka mmoja kwa kampuni za Sanlam General Insurance, Tanzania Insurance Company Ltd, Mgen Tanzania Insurance Company, Real Insurance Tanzania Limited, Reliance Uinsurance Co (T) Limited na Alliance Insurance Corporation Limited ili kujihakikishia usalama wa bidhaa zake wakati wa majanga kama ya moto na mengineyo.

Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, bilioni 1 inayotakiwa kulipwa ipo ndani ya mikataba yote ambayo Gulf iliingia kwa kipindi ha Agosti 15 mwaka 2007 hadi Agosti 15 mwaka 2008.

Tukio la upotevu wa mafuta lilitokea tarehe 28 Mei 2008 wakati Gulf ikiwa bado na mikataba na kampuni zote sita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live