Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni nyingi zaidi Tanzania kuuza Maharage ya Soya China

06066de0d0d7b9803e9071742e3c2153 Kampuni nyingi zaidi Tanzania kuuza Maharage ya Soya China

Tue, 15 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Kampuni 16 kutoka Tanzania zimepata kibali cha kuuza maharage ya soya nchini China na kufanya idadi ya kampuni zinazoingiza na kuuza soya katika taifa lenye watu wengi zaidi duniani kufikia 65.

Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Tanzania nchini China mapema Jumanne imesema kampuni hizo sasa zimeidhinishwa kuuza soya nchini humo.

Mahitaji ya soya nchini China yameongezeka kwa zaidi ya tani milioni mbili katika kipindi cha matazamio ya mwaka 2021-22 na kufikia tani milioni 102 kutoka tani milioni 100.4 zilizo kadiliwa mwaka 2020-21.

China inashikiria zaidi ya asilimia 60 ya biashara ya soya ulimwenguni.

Orodha iliyowekwa kwenye ukurasa rasimi wa twitter wa ubalozi wa Tanzania nchini china imetaja kampuni hizo kuwa ni pamoja na Afagri Global Limited (Dar es Salaam), Afrisian Ginning Ltd (Dar es Salaam), Afrosia International Ltd (Dar es Salaam), BNN Group Ltd (Dar es Salaam), Cochin Dar Impex Ltd (Dar es Salaam), Elements Limited (Dar es Salaam), Examine Africa Company Ltd (Arusha) and GNM Tanzania International Ltd (Dar es Salaam).

Others includes, Kaizen Holding Ltd (Dar es Salaam), Kilimo Umoja Co. Ltd (Dar es Salaam), Paramount Commodities Ltd (Dar es Salaam), RBST international Agribusiness Ltd (Mtwara), Somani Agro Export Ltd (Dar es Salaam), Togabe Co. Ltd (Dar es Salaam), URHOME Co. Ltd (Dar es Salaam) and Tanzaland Textil ltd (Dar es Salaam).

Mwezi April mwaka huu kampuni 49 za kitanzania ziliidhinishwa na Mamlaka ya Forodha Nchini China ili kuuza Maharage ya Soya (Soya Beans) kutoka Tanzania.

Maamuzi hayo yalitokana na mkataba uliosainiwa baina ya Tanzania na China mwezi Oktoba, 2020

Hadi Machi 2021, Tanzania imefanikiwa kusafirisha tani 142 za Maharage ya Soya China na inatarajia kusafirisha zaidi ya tani 13,000.

Chanzo: www.habarileo.co.tz