Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni nne kubangua tani 7,500 za korosho

35781 Koroshopic Kampuni nne kubangua tani 7,500 za korosho

Fri, 11 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtwara. Serikali imetiliana saini mkataba na kampuni nne kwa ajili ya kubangua tani 7,500 za korosho.

Uzinduzi wa ubanguaji huo utafanyika kesho Ijumaa Januari 11, 2019 na naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya.

Kampuni hizo na kiasi cha korosho watakachopatiwa katika mabano ni kiwanda cha Hawte (tani 1,500), Micronix ( 1,200), Korosho Africa Tunduru (2,500) na Micronix Newala (2,400)

Akizungumza leo Alhamisi Januari 10, 2019  Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amezishukuru kampuni hizo kwa kukubali kushauriana na Serikali hadi kufikia makubaliano ya kubangua korosho, akibainisha kuwa mkataba huo ni wa miezi sita.

“Mwisho wa yote tunataka tuje tuuze hizi korosho nje ya nchi na nyingine ndani ya nchi. Ni lazima ziwe katika  viwango vinavyokubalika kimataifa,” amesema Hasunga.

Amesema mbali na kampuni hizo kubangua korosho, Serikali itachukua kiwanda kingine cha Agro Focus kilichopo Newala, kiwanda cha Lindi cha Buco nacho kimeanza majaribio.

Mwakilishi kampuni ya Export Trade Group, Frank Mtui  amesema viwanda walivyo navyo vina uwezo wa kubangua korosho tani 12,500 kwa mwaka lakini kuchelewa kuanza kazi huenda wakafikia tani 10,000.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz