Kampuni ya OpenAI inatarajiwa kumtangaza Emmett Shear kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mpito ikiwa ni saa 48 baada ya kumfukuza kazi bosi na mwanzilishi mwenza Sam Altman.
Bodi ya OpenAI ilimfukuza Alman siku ya Ijumaa juma lililopita kwa kile ilichoeleza kuwa haina imani naye na kumtangaza Mkurugenzi wa Teknolojia wa OpenAI, Mira Murati kama mkurugenzi mtendaji wa muda.
Altman alikuwa na mchango mkubwa katika kuzindua teknolojia ya akili mnemba, ChatGPT.
Kulikuwa na tetesi kwamba huenda Altman angerejeshwa katika nafasi hiyo kutokana na shinikizo la wafanyakazi pamoja na wawekezaji, lakini uwezekano huo unazidi kupungua huku Shear akitarajiwa kurithi mikoba yake.