Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni 8 zawania ujenzi barabara Tanzam

Lami Barabaraaaa Kampuni 8 zawania ujenzi barabara Tanzam

Sun, 23 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema wamepokea makampuni nane ya ukandarasi kutoka mataifa mbalimbali yaliyoomba zabuni ya ujenzi wa barabara kuu ya Tanzania na nchi jirani ya Zambia (Tanzam).

Barabara hiyo inatoka Igawa Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya mpaka Mamlaka ya Mji mdogo wa Tunduma Mkoa wa Songwe yenye urefu wa kilometa 218.

Homera amesema jana Jumamosi, Oktoba 22, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya makandarasi wa kampuni hayo kufika kujitambulisha rasmi ofisini kwake.

Homera amesema mradi huo utakuwa wa barabara ya njia nne sambamba na ujenzi wa miundombinu ya njia za juu katikati ya Jiji la Mbeya jambo ambalo litakuwa mwarobaini wa kupunguza msongamano wa magari yanayoingia na kutoka kwa shughuli za kiuchumi.

“Tunashukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuangalia Mkoa wa Mbeya kuleta fedha kwa ajili ya upanuzi wa miundombinu ya barabara kuu ambayo ni lango la kiuchumi kwa mataifa mbalimbali ni uhakika wangu itakuwa mkombozi na kupunguza ajali.

“Kwa sasa makandarasi hawa wamekuja kuangalia hali halisi ya Maeneo ambayo mradi utapita hususan upatikanaji wa kokote,saruji na rasilimali nyingi na baada ya hapo tunatarajia Novemba 5, 2022 kujua ni kampuni gani imepata tenda ya ujenzi wa barabara hiyo,” amesema.

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Masige Matari amesema upabuzi wa ujenzi wa mradi wa barabara hizo itakuwa mwarobaini wa kupunguza msongamano wa magari na ajali za mara kwa mara.

“Niwatake wananchi wa Mkoa wa Mbeya kuwa watulivu wakati mradi huu ukielekea katika utekelezaji. “Lengo kuu la Serikali ni kuona miundombinu na watu wanakuwa salama katika kuchochea shughuli za kiuchumi ndani na nje ya nchi kutokana na umuhimu wa barabara ya Tanzania na Zambia (Tanzam),” amesema.

Naye Kaimu Meneja wa Tanroad Mkoa wa Songwe, Mhandisi Suleiman Bishanga amesema kuwa upanuzi wa barabara hiyo itaongeza ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika mikoa ya Mbeya na Songwe kutokana na mwingiliano wa kibiashara kupitia mipaka ya nchi jirani za Malawi, Zambia kwenda mataifa mengine.

Mfanyabishara wa sukari, Zena Yusuph amesema kuwa ni wakati sasa Serikali kupanua wigo wa ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na nchi za jirani kwa kuboresha mazingira wezeshi ya Mawasiliano ya barabara reli na anga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live