Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni 500 kushiriki maonyesho Mara

F08BD3C0 BDBA 46FB 92AA F4B729F836C6.jpeg Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo ( TCCIA) Mkoa wa Mara, Boniphace Ndengo

Tue, 19 Jul 2022 Chanzo: Mwananchi

Zaidi ya kampuni 500 kutoka ndani na nje ya nchi zinatarajiwa kushiriki katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya ‘Mara International Business Expo’ yatakayofanyika mkoani Mara mwezi Septemba mwaka huu.

Maonyesho hayo yanayoandaliwa na Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda wa Viwanda na Kilimo (TCCIA) kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Karume mjini Musoma kwa muda wa siku 11.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Musoma leo Julai 19,2022, Mmwemyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mara, Boniphace Ndengo amesema kuwa maonyesho hayo yanalenga kuleta wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kuja mkoani Mara kuzungumza kwa pamoja kuhusu biashara na uwekezaji.

Amesema kuwa wameamua kuandaa manonyesho hayo kutokana Na mkoa wa Mara kuwa na fursa nyingi za kiuchumi ambazo bado hazijatumika vizuri katika kuinua uchumi wa wakazi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.

"Tuna fursa ya ziwa Victoria, hifadhi bora Afrika ambayo ni Serengeti, mkoa wa Mara ni wa pili kwa uchimbaji wa dhahabu na mambo mengi kwahiyo tumeona kuna sababu ya kuiambia dunia kuwa Mara ni bustani iliyo pembeni itembeleeni" amesema

Amesema kuwa wametoa mialiko kwa balozi mbalimbali nchini ambapo hadi sasa ubalozi wa Zimbabwe umethibitisha kushiriki huku akisema kuwa ili kufanikisha maonyesho hayo wabunge wote wa mkoa wa Mara wamekubali kuwa walezi wa shughuli hiyo.

Amesema kuwa maonyesho hayo mbali na kutarajiwa kuleta wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kufika na kujionea fursa za uwekezaji lakini pia yatatumika kama jukwaa kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kujifunza mbinu mbalimbali za kufanya biashara ili waweze kukukuza shughuli zao.

"Tanataka kuutangaza Mkoa wa Mara kama eneo jipya la uwekezaji katika ukanda huu wa Afrika Mashariki kwasababu mkoa unazo sifa hizo hivyo sisi kama sekta binafsi tumeona kuwa tunalo jukumu la kuhakikisha kuwa fursa zilizopo zinawanufaisha wana Mara na Tanzania " amesema

Katibu tawala msaidizi Uchumi na Uzalishaji mkoa wa Mara, Dk Noel Komba amesema kuwa mkoa unatarajia kutumia maonyesho hayo katika kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo mkoani humo.

"Kama mnavyojua tumezindua muongozo wa uwekezaji katika mkoa wetu, kwenye huo mwongozo kuna fursa nyingi sisi kazi yetu itakuwa ni kutafsiri fursa hizo kwa wawekezaji ili ziweze kutumika kwa majufaa ya mkoa wetu" amesema

Mbunge wa jimbo la Musoma Mjini (CCM), Vedastus Mathayo amesema kuwa maonyesho hayo yanatarajiwa kuufungua mkoa wa Mara ambao kibiashara umekuwa nyuma licha ya kuwepo fursa za biashara.

Chanzo: Mwananchi