Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni 16 za Tanzania ‘kuvamia’ soko la China

China Kampuni.png Kampuni 16 za Tanzania ‘kuvamia’ soko la China

Fri, 13 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) Profesa Ulingeta Mbamba amesema jumla ya kampuni 16 yamejisajili kwenda kutangaza bidhaa zao kwenye maonyesho ya sita ya kimataifa nchini China (CIIE)

Maonesho hayo yaliyoanzishwa tangu mwaka 2018, hadi sasa mataifa 51 yameshiriki kwa kuonesha bidhaa zao. Na kwamba kwa mwaka huu maonesho hayo yanatarajiwa kuanza Novemba mosi, katika mji wa Shanghai.

Akizungumza Dar es Salaam leo Oktoba 12 kwenye hafla ya kuwaaga wafanyabiashara hao katika, Ofisi za Ubalozi wa China, Profesa Ulingeta amesema bado wanaendelea kusajili wa wafanyabiashara wenye nia ya kwenda kushiriki maonesho hayo.

"Kampuni 16 yameisha jisajili, tunayo mengi nchini, milango iko wazi bado tunaendelea kusajili mwisho ni Oktoba 17 kabla ya kusafiri, wito wangu wajitokeze kwa wingi soko la China ni kubwa na wateja ni wengi," amesema Profesa Ulingeta.

Amesema ni muhimu kwa Watanzania kulitumia soko hilo katika kufungua fursa kwa kutangaza bidhaa zao zinazozalishwa katika kulifikia soko la China na funia kwenye bidhaa za kilimo,madini na utalii.

Naye mmoja wa wafanyabiashara kutoka kampuni ya Kibisa Millenium Venture, inayouza bidhaa ya kahawa, Stella Magori amesema kwakuwa ni mara yao ya kwanza kushiriki katika soko hilo watapeleka bidhaa za mazao ya kilimo.

"Matarajio yetu ni kupata masoko na wawekezaji na kupata wafu wakushirikiana kupata fursa mbalimbali kwani kila kampuni ina malengo ya kukua tunaamini kufanya hivyo itakuwa chachu kukua kimtaji," amesema

Kwa upande wake, Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian, amesema kadri miaka inavyokwenda maonesho hayo yameendelea kuwa bora na ya mfano kwa kuwa yanakusanya bidhaa kutoka mataifa mbalimbali.

"China bado inatoa kipaumbele kwa mataifa ya Afrika kupeleka bidhaa zake katika soko hilo kuzitangaza ili wapandishe thamani na bei kwa mazao wanayozalisha, lakini bidhaa zao zinahitajika zaidi," amesema.

Amesema China ni soko kubwa na la pili kwa ukubwa kwa bidhaa kutoka Afrika huku akieleza kutokana na kasi ya ukuaji wa maonesho hayo ya sita muda si mrefu watakuwa wanaongoza.

Amesema katika kipindi cha miaka yote sita tangu kuanzishwa kwa maonesho hayo Tanzania imekuwa ikishiriki kuonyesha bidhaa mbalimbali ikiwemo korosho, soya na bidhaa zingine za kilimo.

"Kwa mwaka 2022 jumla ya tani 1000 za Soya zilipelekwa China na hata mwaka huu tangu Januari hadi Agosti jumla ya tani 2000 zimepelekwa hii ni kwa mujibu wa masoko ya wafanyabiashara China," amesema

Amesema kuendelea kukua huo ni ishara kuwa Tanzania ni miongoni mwa mataifa ya Afrika yanayotumia fursa ya soko la China ambalo lina wateja wengi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live