Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni 150 kushiriki maonesho ya ubunifu

Kampuni 150.png Kampuni 150 kushiriki maonesho ya ubunifu

Wed, 11 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya kampuni 150 za wabunifu zitashiriki maonesho ya ubunifu yatakayofanyika tarehe 13 na 14 Oktoba mwaka huu katika makubusho ya Taifa jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Sahara Venture, Musa Kamata amesema.

Amesema maonesho hayo yenye jina la Sahara Spacks ni tukio linalojihusisha na masuala ya ubunifu, ujasiliamali,uwekezaji na teknolojia ambapo tangu mwaka 2016 wamekuwa wakiandaa tamasha hilo.

“Na mwaka huu tumejipanga vizuri na tuna mikakati tofauti lengo kubwa tunataka kuonesha nini vijana wa kitanzania wanataka kufanya, tutakuwa na maonesho ambayo yataanza ijumaa ya wiki hii na jumamosi Makumbusho ya Taifa lakini tunashukuru kwa sapoti kutoa serikali na kutoka tume ya taifa ya sayansi na teknolojia wamekuwa chachu kubwa kwenye masuala ya ubunifu,” ameeleza.

Amebainisha kuwa lengo la maonesho hayo ni kuhakikisha wanawashirikisha wadau mbalimbali kwani kuna mabadiliko mengi na teknolojia inakua na vitu vimebadilika hivyo wanahakikisha watanzania wanaenda nayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live