Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni 14,000 zawasilisha taarifa

Kampuni Pixc Data Kampuni 14,000 zawasilisha taarifa

Wed, 5 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumla ya kampuni 14,026 zimewasilisha taarifa za wamiliki manufaa wa kampuni (Beneficial owners) katika kampuni zilizosajiliwa nchini.

Licha ya idadi hiyo bado uwasilishwaji huo umeonekana kujivuta kwani kuna zaidi ya kampuni 140,000 ambazo zinafanya idadi ya waliowasilisha kuwa asilimia 14 tu ya ilivyotarajiwa.

Kufuatia hali hiyo Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo amewaongezea muda wa uwasilishwaji wamiliki hao ambapo wanatakiwa kuwasilisha taarifa hizo kuanzia Januari hadi Juni 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa leo Jumanne Jauari 4, Profesa Mkumbo amesema katika kufanya marekebisho ya Sheria kifungu cha 45(A) kilizitaka kampuni kuanza kuwasilisha taarifa za wamiliki wa makampuni ambapo makampuni yalipewa muda wa miezi sita yawasilishe taarifa hizo kutoka Juni 2021 hadi Disemba 2021.

“Kanuni za kutekeleza sheria hii zilikamilika mwaka jana mwezi Mei na Makampuni yalipewa miezi sita yawe yamewasilisha taarifa hizo,,, kutokana na upya wa dhana ya umiliki wa manufaa Makampuni mengi hayakuweza kuwasilisha taarifa zao na yameomba kuongezewa muda”alisema

Profesa Mkumbo amesema kutokana na changamoto zilizojitokeza na kuzingatia maombi ya wafanyabiashara kuongezewa muda wa kuwasilisha taarifa husika, aliamua kuongeza muda wa uwasilishwaji kwa mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 459A (2) cha Sheria ya Makampuni sura ya 212.

Aidha Mkumbo amesema kupitia kwa wakala wa usajili wa Biashara na leseni (BRELA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeanza kutekeleza zoezi la sensa ya Makampuni lililoanza Disemba 2021 na kukamilika mapema Februari 2022 ikiwa ni mara ya kwanza kuanza zoezi hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live