Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamati yapewa elimu ukokotoaji wa bei bidhaa za Mafuta

Screenshot 20240528 070612 Collage Maker GridArt Kamati yapewa elimu ukokotoaji wa bei bidhaa za Mafuta

Tue, 28 May 2024 Chanzo: dar24

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wamepewa elimu ya ukokotoaji wa bei za bidhaa za mafuta nchini, iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji – EWURA.

Elimu hiyo imetolewa Mei 27, 2024 jijini Dodoma ambapo Wabunge hao walipata nafasi ya kujifunza namna tofauti za ukokotoaji wa bidhaa ya mafuta nchini, huku Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi kutoka EWURA, Msafiri Mtepa akusema bei za mafuta nchini hupangwa kwa kutumia kanuni ya kupanga bei za nafuta ya mwaka 2022.

Amesema, kanuni hiyo imekuwa ikifanyiwa marekebisho na mabadiliko mbalimbali yanayohusu upangaji wa bei za mafuta hapa nchini, ambapo bei za mafuta zinapangwa kila mwezi na kuchapishwa katika Gazeti la Serikali baada ya kupitishwa na Bodi ya EWURA.

Mtepa pia amesema utayarishaji wa kanuni hizo hushirikisha wadau wote muhimu wakiwemo Wananchi, huku akizitaja sababu zinazosababisha kupanda kwa bei ya mafuta nchini kuwa ni pamoja na madhara ugonjwa wa Corona ambao umesababisha kupungua kwa hifadhi ya mafuta duniani.

Sababu nyingine ni hali ya usafirishaji wa mafuta kuwa mbaya na kupungua mahitaji ya mafuta pamoja na thamani ya fedha kushuka kutokana na kuanza kwa Vita ya Urusi na Ukraine.

Kwa Upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Kilumbe Ng’enda ameitaka EWURA kuendelea kusimamia vizuri mwenendo mzima wa upatikanaji wa mafuta, kusimamia bei za mafuta na kudhibiti upandaji wa bei ya bidhaa hiyo nchini.

Kwa Upande wake Naibu Waziri Wa Nishati, Judith Kapinga amesema Wizara itafanyia kazi ushauri wote uliotolewa na kamati, ili kuweza kuboresha huduma ya upatikanaji wa mafuta na udhibiti wa bei ya mafuta nchini.

Chanzo: dar24