Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamati ya Majaliwa kuhusu bei ya mafuta yamaliza kazi

1f3a49b0f91fb4d68cd675cf8d638c02 Kamati ya Majaliwa kuhusu bei ya mafuta yamaliza kazi

Mon, 27 Sep 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI imesema kamati iliyoundwa na Waziri Mkuu kutathmini bei ya mafuta imemaliza kazi na ilipangwa imkabidhi ripoti Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa juzi lakini ilishindikana.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alisema jana kuwa, uteuzi aliofanya Rais Samia Suluhu Hassan juzi wa viongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) uliigusa kamati hiyo iliyokuwa ikijiandaa kuwasilisha taarifa yake.

Msigwa alisema hayo mjini Singida jana alipokuwa akitoa taarifa ya wiki kuhusu utendaji wa serikali.

“Kama mnavyofahamu mamlaka ya uteuzi jana (juzi) alifanya uteuzi wa viongozi na uteuzi huo umegusa baadhi ya taasisi ambazo Mheshimiwa Waziri Mkuu alikuwa akutane nazo na kutoa maelekezo ya serikali hivyo siku mbili tatu taarifa hiyo itatolewa,” alisema.

Mwanzoni mwa mwezi huu, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) ilitangaza bei mpya za mafuta ya petrol na dizeli lakini serikali ilisitisha uamuzi huo.

Msigwa alisema serikali baada ya kupokea taarifa hiyo itatoa muongozo kuhusu jambo hilo. Ewura ilitangaza ongezeko la bei ya mafuta kwa madai ya kupanda kwa bei kwenye soko la dunia.

Chanzo: www.habarileo.co.tz