Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamati ya Bunge yatoa neno TANTRADE

Saba2 Sehemu ya Mamlaka ya biashara ya nje, TanTrade

Wed, 16 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imefanya ziara katika Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na kukagua miundombinu ya uwanja wa maonesho wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (sabasaba).

Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati David Kihenzile ameupongeza uongozi wa TanTrade kwa jitihada unazofanya katika kusimamia biashara nchini na hasa namna ulivyoweza kufanikisha ushiriki wa Tanzania katika maonesho ya Dunia ya Expo2020 Dubai.

Kupitia maonesho hayo , Tanzania ilifanikiwa kusaini jumla ya mikataba 36 yenye thamani ya shilingi trilioni 17.35, ambapo utiaji saini wa mikataba hiyo ulishuhudiwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Uwekezaji ,Viwanda na Biashara Exaud Kigahe ambaye aliongozana na Wajumbe wa Kamati hiyo ameahidi kuyafanyia kazi mapendekezo yao ikiwa ni pamoja na kufanya maboresho ya uwanja wa maonesho wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ili uwe na miundombinu ya kisasa na iweze kuvutia Wafanyabiashara wengi zaidi kutoka ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Latifa Mohamed Khamis amesema, mpaka kufikia mwezi Februari mwaka huu, Mamlaka hiyo imefanikiwa kupata soko la nyama nchini Qatar tani 120 za nyama ya mbuzi, Saudi Arabia tani 100 za nyama ya ng’ombe kwa mwezi pamoja na kuwakutanisha wazalishaji wa nafaka, muhogo, soya, asali, viungo, bidhaa za ngozi, chai na kahawa kuweza kuyafikia masoko ya nje ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live