Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamati ya Bunge yamulika ujenzi Bandari ya Uvuvi Kilwa

Kilwa Pichnj Kamati ya Bunge yamulika kasi ya ujenzi Bandari ya Uvuvi Kilwa

Fri, 17 Mar 2023 Chanzo: mwanachidigital

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara, Kilimo, Mifugo na Uvuvi imesema haijaridhiishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa na kuitaka Serikali na mkandarasi wa ujenzi wa mradi kuongeza kasi ya ujenzi ili uweze kukamilika kwa wakati kama ulivyopingwa.

Akizungumza baada ya kamati hiyo kusomewa taarifa na kufanya ukaguzi wa eneo la ujenzi mwenyekiti wa kamati hiyo David Kihonzile amesema hajaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huyo ambao umepangwa kukamilika mwenzi Septemba 2024.

"Kamati imesomewa taarifa na kukakagua eneo la ujenzi wa bandari lakini hatujaridhika na mwenendo wa kasi ya ujenzi tumeiangiza Serikali kusimamia kwa ukaribu mradi huu ili uweze kukamili mapema kama ilivyokusudiwa,” amesema Kihenzile ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo.

Aliongeza kuwa serikali ni vyema wakawa waangalifu wakati wa ulipaji fidia maeneo ya wananchi ili kusiwe na malalamiko.

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdala Ulega amesema kuwa wamepokea ushauri wa kamati na watasimamia utatuzi wa changamoto zilizopo kwa ukaribu ili mradi ukamili kwa wakati kama ulivyokusudiwa.

"Serikali ya Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ameamua kwa vitendo kusimamia ujenzi wa miradii mikubwa ikiwemo wa ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa ili kutatua tatizo la ajira kwa vijana na kuongeza uchumi wa nchi,” amesema Ulega.

Ulega amesema kuwa gharama ya ujenzi wa mradi huo mpaka kukamilika utatumia Sh282 bilioni na unatarajia kukamilika Septemba 2024 na tayari fedha Sh50 bilioni zimetengwa kwa ajili ya kuendelea kulipa gharama za mradi.

Chanzo: mwanachidigital