Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamati ya Bunge yakoshwa na kasi ujenzi viwanja wa ndege

4ae1cac7dbefd4690aa6865b038bc03d Kamati ya Bunge yakoshwa na kasi ujenzi viwanja wa ndege

Wed, 16 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeipongeza Serikali kwa kupitia Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzanai (TAA), kwa kukamilisha mradi wa ujenzi wa uzio katika kiwanja cha ndege cha Mwanza ili kuongeza

usalama wa kiwanja hicho.

Akizungumza jijini Mwanza mara baada ya kukagua mradi huo ambao umejengwa na Kampuni ya M/s Mumangi Trans & Construction, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Selemani Kakoso, amesema kukamilika kwa hatua hiyo

kutapunguza matukio ya ajali ambazo zimekuwa zikiripotiwa kiwanjani hapo.

“Niipongeze sana Serikali kwa kutoa fedha na kukamilisha mradi huu, maana kulikuwa na matukio ya ajali za wanyama na binadamu na nina imani kwa sasa hatutasikia tena matukio ya ajali",” amesema Kakoso.

Kakoso ameitaka TAA kuhakikisha inaweka mipaka katika maeneo ya viwanja vyao vyote nchini na kuvitafutia mapema hati miliki ili kuepuka uvamizi na kupunguza migogoro kwa wananchi kwenye maeneo ya

viwanja vya ndege.

“TAA mna maeneo makubwa sana kwenye viwanja lakini havina hati miliki mfano Sumbawanga, Mtwara, Songea na maeneo mengine na wananchi wanasogea taratibu msipokaa sawa mtajikuta mnapelekwa mahakamani na

kiwanja ni cha kwenu,”amefafanua Mwenyekiti Kakoso.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Atupele Mwakibete, amesema Serikali imejipanga kutekeleza miradi ya maboresho kwa kiwanja cha ndege cha Mwanza ili kuupa hadhi uwanja huo

kulingana na taratibu za usafiri wa anga.

Naye, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Hamisi Amiri, amesema ujenzi wa uzio kwa sasa umekamilika kwa asilimia mia moja na umegharimu takribani bilioni mbili.

Mkurugenzi Amiri ameongeza kuwa ujenzi wa uzio umezingatia viwango vya sasa vya Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO), ili kuendana na hadhi na kiwanja hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live