Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamati ya Bunge yaitaka serikali kufanya utafiti sekta ya mafuta na gesi

Tue, 19 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Kamati ya Bunge ya Bajeti imeishauri Serikali kufanya utafiti na kuona nini hasa kimechangia kupungua kwa shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi nchini.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Hawa Ghasia amesema bungeni leo Juni 18 2018 wakati akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo kuhusu hali ya uchumi na Mpango wa Taifa wa Maendeleo na bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19.

“Kamati inaishauri Serikali kufanya tafiti na kuona nini hasa kimechangia kupungua kwa shughuli za utafutaji mafuta na gesi na nini kifanyike kwa haraka kurekebisha kasoro hiyo na hivyo kuendelea kupata mapato kutoka katika sekta ya gesi,”amesema.

Amesema sura ya bajeti inatakiwa ionyeshe kiasi cha mapato yaliyopatikana kwenye shughuli za utafutaji na uwekezaji wa mafuta na gesi.

Ghasia amesema takwimu zinaonesha shughuli za utafutaji na uwekezaji wa mafuta na gesi  zinapungua siku hadi siku na hivyo kushindwa kukidhi matarajio ya Serikali kwa sekta hiyo kuchangia bajeti ya Serikali.

“Hivi karibuni tumeshuhudia kampuni kubwa ya kimarekani ya Exxon Mobil ikionesha nia ya kuuza visima vyake vya gesi nchini ilianza mchakato wa kuwekeza kwa njia ya kuchangia mtaji katika mradi wa LNG Likongo mkoani Lindi,”amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz